Radio Rahma - Home

Studio Contacts: 0721108666 / 0713230198 (SMS)
Taarifa Za Habari - Click Hapa | Follow us Our Facebook Page Our Twitter Account

Marehemu Profesa Ali Mazrui alizaliwa mjini Mombasa 24 Februari mwaka 1933.

Ameacha wajane wawili mmoja raia wa Uingereza na mwingine raia wa Nageria pamoja na watoto watano.

Kabla ya kifo chake Marehemu Mazrui alikuwa mhadhiri katika chuo kikuu cha Binghamton mjini New York. Aidha alijudumu kama chansela wa kwanza wa chuo kikuu cha Jomo Kenyatta chini ya uongozi wa aliyekuwa rais Kibaki.

Kwa miaka mingi Mazrui alisikizwa na viongozi wa mataifa mengi ya afrika na ya kigeni, akizungumzia nafasi ya Afrika katika dunia nzima.

Alichapisha vitabu vingi na pia kuandika nyaraka mbali mbali kuhusu siasa za Afrika, athari za siasa kwa dini ya kiisilamu na uhusiano kati ya mataifa ya Kaskazini na Kusini.

Alipigia debe wazo la Afrika kuwa huru na alikosoa mataifa yanayonyakua rasilimali za Afrika na kunyanyasa watu wake.

Kwa miaka kumi alikuwa katika chuo kikuu cha Makerere , Kampala, Uganda, ambako alihudumu kama mkuu wa idara ya mswala ya siasa, kwa wakati mmoja alihudumu kama naibu rais wa muungano wa kimataifa wa maswala ya siasa na amekuwa mhadhiri katika kontinenti 5.

Dr. Mazrui pia aliwahi kuhudumu kama mshauri maalum wa benki wa dunia na pua akahudumu katika bodi ya wakurugenzi ya baraza la waislamu nchini Marekani.

 

----- §§§ -----

Featured Partner

Want to Advertise? Call Us On
0713791483 or 0738583642