Mratibu wa kitaifa chama cha kijamii cha GEMA Eliud Mbega ameitaka jamii nchini kuwa na umoja msimu huu wa uchaguzi ili kuwachagua viongozi bora.

Akizungumza kwenye kongamano lililowaleta pamoja wakilishi mbalimbali wa jamii hiyo Mbega ameitaka jamii ya GEMA kulinda umoja wao na kuhakikisha kuwa wanajitokeza kwa wingi katika zoezi la kupiga kura.

Kulingana naye umoja ndio suluhu la chaguo la kiongozi bora.Jamii ya GEMA ambayo ni mkusanyiko wa kabila tofauti ikiwemo Waembu,Meru na Gikuyu sasa wameuidhinisha mwaniaji wa ugavana kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir kuchukua uongozi wa kaunti.

Kulingana nao Nassir ndiye kiongozi pekee ambaye ana tajriba ya uongozi na kwamba wana Imani kuwa maslahi jamii ikiwemo jamii hiyo yatatekelezwa.