Mashirika ya kutetea haki za kibindamau katika kaunti ya Kilifi yameelezea kushangazwa na ongezeko la visa vya ajali barabarani miongoni mwa wanabodaboda.

Mashirika hayo yamesema kuwa wanabodaboda takriban kumi kufariki kwenye ajali zinazohusisha magari na bodabodandani ya mwezi mmoja.

Afisa wa shirika la Kilifi Social Justice Center Eric Mgoja amesema kuwa baadhi ya ajali hizo zinaweza kuepukika iwapo wanabodaboda hao watapata mafunzo ya kuendesha magari na bodaboda.

Mgoja amesema kuwa matrela ndiyo ambayo huuwa wanabodaboda hao hasa kwenye barabara kuu ya Mombasa Malindi na Mombasa Nairobi.

Afisa huyo amewataka viongozi kuingilia kati na kudhamini wanabodaboda hao ili waendeleze mafunzo ya udereva kwani wengi wao wanatoka jamii maskini na hawawezi kumudu fedha za mafunzo hayo.