Familia moja kutoka eneo la Guraya Bibi wa Shafi inalilia haki baada ya nyumba yao kuvunjwa kwa njia ya kutatanisha.

Kulingana na Mzee Mwinyi Kibwana, nyumba hiyo ilinunuliwa zaidi ya miaka 30 iliyopita na ilikuwa imejengwa kwenye ardhi iliyo chini ya himaya ya serikali.

Mzee Mwinyi anaeleza kuwa Mzozo uliibuka baina yake na bwenyenye mmoja baada kuanza kulipia ardhi hiyo kwa serikali.

Aliyekuwa meya wa Mombasa Rajab Sumba anasema kuwa Mzozo wa kipande hicho cha ardhi ulianza miaka ya nyuma baada ya tofauti kuibuka baina ya babake bwenyenye huyo na familia ya mzee Mwinyi kuhusu malipo ya kipande hicho.

Kwa upande wake mkereketwa wa maswala ya kijamii eneo bunge la Mvita Hassan Rajab amesikitishwa na ubomozi huo uliotekekezwa mwendo wa saa kumi na moja alfajiri siku ya Jumamosi.

Mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi aliyezuru eneo la mkasa amekemea vikali kitendo hicho akitaja kuwa ilikuwa kinyume na sheria ikizingatiwa kuwa kesi inayohusiana na ardhi hiyo ingali mahakamani huku akiwataka waliotekeleza ubomozi huo kulipa fidia.