Wanawake wanaowania nyadhifa mbali mbali za kisiasa, wametakiwa kupigania nyadhfa hizo hadi uchaguzi mkuu ujao.

Kulingana na mkurugenzi mkuu wa chama cha wanawake wanahabari nchini AMWIK, Judy Kaberia, amewarai wanawake kusimama kidete na kupambana kisiasa na wenzao wa kiume bila ya uoga wa kudhulumiwa.

Kaberia vile vile ameonya dhidi ya dhuluma za aina mbali mbali wanazopitia wanawake wawaniaji wakati huu, akisema hilo lisiwe chanzo cha kuwarudisha nyuma katika safari yao ya uongozi.

Huku hayo yakijiri Wito umetolewa kwa wakaazi wa kaunti ya Taita Taveta kuwachagua viongozi kike wanaowanaia nyadhfa mbali mbali kaunti hio kama njia moja wapo ya kubadilisha uongozi.

Wakereketwa wa mswala ya siasa, kutoka maeneo ya wadi ya Wusi/Kishamba wakiongozwa na Lydia Wakesho wamesema kuwa wakati mwingi hasa kaunti ya Taita Taveta uongozi umekuwa wa jinsia ya kiume na kusema kuwa imefikia wakati sasa wanawake wanaowania nyadhfa kupewa nafasi.

Wakesho amesema kwamba kumekuwa na viongzi wanawake ambao wamekuwa wakijitokeza kugombania lakini wananachi wamekosa hamasa kuhusu uongozi wa akina mama.

Wakesho ameongeza kuwa kwa sasa kuna viongozi wengi wanaojitokeza na kuendelea kutoa wito kwa wananchi kaunti ya Taita Taveta kutojiingiza kwenye siasa za vurugu na badala yake, kuendelea kudumisha amani.