Hatimae mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini jenerrali Francis Ogolla amezikwa katika eneo la Ng’iya kaunti ya Siaya.
Ogollah amezikwa kwa kuzingatia heshima na taratibu zote za kijeshi kama vile kupigwa kwa mizinga 19 iliyopigwa na wanajeshi wanamaji yaani navy.
Jenerali Ogollah amezikwa ndani ya saa 72 baada ya kifo chake kilichotokea siku ya Alhamisi kufuatia ajali ya ndege ya helikopta alimokuwa akisafiria pamoja na wanajeshi wengine 10.
Katika wosia wake marehemu Ogolla alitaka azikwe ndani ya muda mchache baada ya kifo chake na mazishi yenyewe yawe ya kawaida sana.
Akizungumza wakati wa ibada ya kumuenzi jenerali Ogolla iliyoandaliwa katika uwanja wa Ulinzi Sports Complex jijini Nairobi, mwanawe Joe Ogolla alibainisha kwamba jeneza lililotumika kumbeba jenarali huyo liligharimu shilingi 6,800.
Hata hivyo jenerali Ogolla hakuzikwa na jeneza hilo kwani katika wosia wake alitaka tu afunikwe na shuka nyeupe wakatati akizikwa.

Maafisa wa upelelezi wa kupambana na mihadarati Mombasa wamemkamata mlanguzi wa dawa za kulevya eneo la Kiembeni, Bombo eneo la Kisauni.
Idara ya upelelezi nchini DCI inasema kuwa maafisa hao wamenasa sacheti kadhaa zinazoshukiwa kuwa na heroini na bangi kutoka kwa nyumba yake na gari lake la kibinafsi.
Mshukiwa huyo, Zuher Ali Mohamed, amekamatwa katika operesheni ya asubuhi na mapema baada ya maafisa hao kupata taarifa kutoka kwa umma.
Gari la mtuhumiwa huyo linaloaminika kupatikana kutokana na uhalifu limekamatwa.
Aidha pesa taslimu shilingi 26, 250 na Dola 200 za Kimarekani, mizani, bahasha za kupakia na simu tatu zinazosadikiwa kuwa na data za wapambe wake pia zimekamatwa.
Atafikishwa katika Mahakama ya Mombasa Aprili 18, 2024.

Seneta mteule wa chama cha UDA hapa Mombasa Miraj Abdillah ametaka wakenya kutomnyoshea kidole cha lawama waziri wa Afya Susan Nakhumicha kuhusiana na mkwamo uliopo katika sekta ya afya humu nchini.

Akizungumza na vyombo vya habari Miraj amesema kuwa waziri Nakhumicha hapaswi kulaumiwa kwani mzigo alioupata katika wizara hio ni mkubwa na anapaswa

kupewa muda kutekeleza majukumu yake.
Seneta huyo ameonyesha kusikitishwa kwake namna swala hili linavyoshughulikiwa na baadhi ya wakenya ikizingatiwa kuwa waziri wa afya ni wa jinsia ya kike.

"Hata sahi tunazungumzia masuala ya mbolea ambayo ni ghushi lakini vile vidole vya lawama vimeelekezwa kwa waziri ni vichache sana. Kwa nini sisi tumekuwa tukujirejelea kuonea jinsia ya kike? Mahali kokote ambapo mwanamke amepewa majukumu ndiko mahali ambapo sisi tunaonyesha udhaifu" Akasema Miraj.

Miraj amesema mkataba wa makubaliano CBA, kati ya serikali na madaktari ulifanyika wakati wa utawala uliopita hivyo basi hivyo basi wanafaa kuwa na subra.
Aidha Miraj ameongeza kuwa madaktari wanafaa kupatia serikali muda wa kulainisha masuala iliyorithi kutoka kwa serikali iliyopita.
Vile vile amewataka madaktari kuwa na utu kwani wakenya walala hoi ndio wanaotaabika wakati wanapoendeleza mgomo.

"Tunatatizika sana na madaktari kutokuwa katika sehemu zao za kazi ikifahamika kwamba wananchi ndio wanaoumia. Nyinyi ni wafanyikazi lakini sio wafanyikazi wa kawaida. Nyinyi ni kama mitume" Akaongeza Miraj.

Inspekta Jenerali wa Polisi, Japhet Koome ametaja maandamano ya madaktari na maafisa wa kliniki kama usumbufu kwa umma.

Kulingana na Koome, watabibu hao wamekuwa wakilala barabarani na hivyo kuzuia barabara kuu, barabara za umma na kutatiza mtiririko wa magari na harakati za watu wakati wa maandamano yao.

Koome amesema kuwa matabibu hao wameshiriki maandamano hayo bila kuwafahamisha maafisa wa polisi, jambo ambalo ni kinyume na sheria za Kenya.
Aidha amesema kuwa wasio madaktari, ambao wana nia ya kusababisha maafa kwa umma wanakusudia kujiunga na maandamano yanayoendelea.

Sasa madaktari wametakiwa kufanya maandamano hayo kwa tahadhari, kwani kitendo chochote cha kuvunja haki za umma hakitavumiliwa.

Kwa hiyo kwa maslahi ya usalama wa taifa, Makamanda wote wa Polisi wameagizwa kushughulikia hali hizo kwa uthabiti na kwa mujibu wa sheria. Tunataka kuwaonya madaktari wote kujiepusha na kukiuka haki za wengine wanapoandamana, na kwamba juhudi zao za kutatiza utendakazi mzuri wa hospitali hazitavumiliwa,” Koome akasema.

Ni mwezi mmoja tangu madaktari waanze mgomo, na wamekuwa wakiandamana kudai kuajiriwa kwa madaktari wanajenzi na utekelezaji wa makubaliano mengine katika CBA ya mwaka 2017.

Kwa upande mwingine, maafisa wa kliniki wako katika wiki yao ya pili ya mgomo, wakitoa matakwa sawa.
Wakiongozwa na miungano yao, Chama cha Madaktari, Wanafamasia, na Madaktari wa Meno (KMPDU) na Muungano wa Maafisa wa Kliniki nchini (KUCO), madaktari hao wameapa kutolegeza Kamba hadi serikali itimize matakwa yao.

Juhudi za serikali, kupitia Wizara ya Afya na Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei, kujadili mbinu ya kurejea kazini kwa madaktari hazijafaulu.

Ni mwezi mmoja tangu madaktari washushe zana zao, na wamekuwa wakiingia barabarani kudai kutumwa kwa wafanyikazi na utekelezaji wa makubaliano mengine katika CBA ya 2017.

Kwa upande mwingine, maafisa wa kliniki wako katika wiki yao ya pili ya mgomo, wakitoa matakwa sawa.

Wakiongozwa na miungano yao, Chama cha Madaktari, Wafamasia, na Madaktari wa Meno (KMPDU) na Muungano wa Maafisa wa Kitabibu wa Kenya (KUCO), madaktari hao wameapa kutolegea hadi serikali itimize matakwa yao.

Juhudi za serikali, kupitia Wizara ya Afya na Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei, kujadili fomula ya kurejea kazini na madaktari hazijafaulu.

Mahakama ya Mombasa imewapa polisi siku 21 kuwachunguza wanaume wawili wanaoshukiwa kuwasajili vijana kujiunga na makundi ya kigaidi katika taifa la Somalia na DRC.
Afisa mpelelezi amemwambia hakimu David Odhiambo kwamba Hussein Yusuf Mrafi na Ali Mwalimu Mwinyi wanashukiwa kuwa wanaajiri watu kuingia ISIS na Al Shabaab.
Wanashukiwa kutenda kosa la Kuajiri Wanachama wa Kundi la Kigaidi kinyume na Kifungu cha 13 cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi nambari 30 ya mwaka 2012.
Maafisa wa upelelezi wanaamini kuwa Mrafi, 27, na Mwinyi, 21, wanaweza kuwa sehemu ya kundi la magaidi katika eneobunge la Likoni, hapa Mombasa linalowasajili vijana kujiunga na magaidi wa ISIS na Al Shabaab katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Somalia.
Afisa wa upelelezi ameiambia mahakama kuwa alihitaji siku 30 kukamilisha upelelezi ikiwa ni pamoja na kuchukua simu tatu zilizokamatwa kutoka kwa mshukiwa wa kwanza kwa uchunguzi wa kitaalamu.
Katika hukumu yake hakimu Odhiambo alimpa mpelelezi siku 21 kukamilisha uchunguzi wake akiagiza kesi hiyo isikizwe tarehe 7 Mei 2024.

Show more post

 

More Stories

Buriani jenerali Francis Ogolla

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo