Hatimae mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini jenerrali Francis Ogolla amezikwa katika eneo la Ng’iya kaunti ya Siaya.
Ogollah amezikwa kwa kuzingatia heshima na taratibu zote za kijeshi kama vile kupigwa kwa mizinga 19 iliyopigwa na wanajeshi wanamaji yaani navy.
Jenerali Ogollah amezikwa ndani ya saa 72 baada ya kifo chake kilichotokea siku ya Alhamisi kufuatia ajali ya ndege ya helikopta alimokuwa akisafiria pamoja na wanajeshi wengine 10.
Katika wosia wake marehemu Ogolla alitaka azikwe ndani ya muda mchache baada ya kifo chake na mazishi yenyewe yawe ya kawaida sana.
Akizungumza wakati wa ibada ya kumuenzi jenerali Ogolla iliyoandaliwa katika uwanja wa Ulinzi Sports Complex jijini Nairobi, mwanawe Joe Ogolla alibainisha kwamba jeneza lililotumika kumbeba jenarali huyo liligharimu shilingi 6,800.
Hata hivyo jenerali Ogolla hakuzikwa na jeneza hilo kwani katika wosia wake alitaka tu afunikwe na shuka nyeupe wakatati akizikwa.


 

More Stories

Vita dhidi ya mihadarati vyapamba moto Pwani

Fuo za bahari sasa ni marufuku

Ufunguzi wa shule waahirishwa kwa muda usiojulikana

Buriani jenerali Francis Ogolla