Maafisa wa upelelezi wa kupambana na mihadarati Mombasa wamemkamata mlanguzi wa dawa za kulevya eneo la Kiembeni, Bombo eneo la Kisauni.
Idara ya upelelezi nchini DCI inasema kuwa maafisa hao wamenasa sacheti kadhaa zinazoshukiwa kuwa na heroini na bangi kutoka kwa nyumba yake na gari lake la kibinafsi.
Mshukiwa huyo, Zuher Ali Mohamed, amekamatwa katika operesheni ya asubuhi na mapema baada ya maafisa hao kupata taarifa kutoka kwa umma.
Gari la mtuhumiwa huyo linaloaminika kupatikana kutokana na uhalifu limekamatwa.
Aidha pesa taslimu shilingi 26, 250 na Dola 200 za Kimarekani, mizani, bahasha za kupakia na simu tatu zinazosadikiwa kuwa na data za wapambe wake pia zimekamatwa.
Atafikishwa katika Mahakama ya Mombasa Aprili 18, 2024.


 

More Stories

Buriani jenerali Francis Ogolla

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo