Naibu kamanda wa polisi katika kaunti ndogo ya Nyali Daniel Masaba amewataka wakaazi wa Mombasa kutotembelea fuo za bahari.
Akizungumza wakati wa shughli ya usafi iliyofanyika katika fukwe ya bahari eneo la Nyali, Masaba amesema marufuku hio itadumu hadi pale hali itakapokuwa shwari.

"Tumeonywa na viombo vya habari kwamba bahari ni mbaya. Kwa ajili hio natoa amri kuanzia sai hakuna mtu anatakikana akuwe ndani ya maji mpaka bahari itulie.", amesema Masaba.
Marufuku hio inatokana na taarifa za kuwepo kwa kimbunga Hidaya kinachotarajiwa kupiga Pwani ya Kenya na mataifa mengine ya Afrika Mashariki yanayopakana na fuo za bahari.
Ikiwa leo ni siku ya kusherehekea siku kuu ya uhuru wa viombo vya habari, Masaba amesifu juhudi za vyombo vya habari nchini.
Aidha amesema kuwa viombo vya habari vinatekeleza wajibu mkubwa wa kufahamisha umma.

"Kwa upande wa usalama, hatuwezi kufanya kazi bila kuwahusisha wanahabari. Huwa wanatupa taarifa na vile vile kutusaidia kutathmini utendakazi wetu", akaongeza Masaba