Dawa za kulevya aina ya Cocaine na Heroine inayokadiriwa kuwa na thamani ya shilingi milioni 3.7 zimepatikana katika operesheni iliyoendeshwa katika maeneo ya Kaunti za Mombasa na Kilifi.
Katika operesheni iliyofanywa mapema leo (Mei 7, 2024) na timu ya pamoja ya Kitengo cha Kupambana na Mihadarati (ANU) na wapelelezi wa Kitengo cha Uhalifu uliopangwa (TOCU), gramu 50 za kokeini na kilo 1.15 za heroini zilipatikana.
Mshukiwa Hussein Mansur Salim amenaswa Kisauni, Mwandoni akiwa na takriban gramu 50 za kokeini zenye thamani ya shilingi 250,000.Huko Kisauni katika eneo la steji ya Paka, Ali Swale pia amekamatwa na takriban kilo 1 ya dawa za kulevya aina ya heroine, zikiwa na thamani ya shilingi milioni 3.
Kadhalika, Harrison Mwenda Kiambi naye alinaswa huko Mtwapa Maweni akiwa na heroini yenye uzito wa gramu 150, thamani yake ikiwa shilingi 450,000.
Washukiwa hao watatu wako chini ya ulinzi wakisubiri kufikishwa mahakamani.

Hayo yakijiri watu saba wamekamatwa mjini Lamu wakiwa na dawa za kulevya aina ya Cocaine yenye thamani ya shilingi milioni 3.7.
Kulingana na idara ya upelelezi wa makosa ya Jinai (DCI), operesheni hio imeoongozwa na mjasusi na timu za kitengo cha kupambana na mihadarati.
Washukiwa hao saba wametiwa nguvuni katika maeneo tofauti ya kaunti ya Lamu katika oparesheni ambayo imepelekea kunaswa kwa takriban gramu 928.
Watuhumiwa hao wametajwa kuwa ni Nuura Omar Bori mwenye umri wa miaka 34, Mote Mwalimu Shamuni (41), Shamuni Mwalimu Shamuni (41), Omar Mohamed Omar (23), Mohamed Abdallah (35) na Fami Abdulrahman Mohamed na Fatma Mote Yusuf (40).
Hivi sasa wamezuiliwa chini ya ulinzi wa polisi wakisubiri kufikishwa mahakamani.