Kongamano la kujadili mbinu za kuboresha uchumi wa baharini baina ya mataifa wanachama wa IGAD limekamilika rasmi hapa jijini Mombasa.
Kongamano hilo la siku nne liliwaleta pamoja wawakilishi kutoka mataifa na taasisi mbali mbali barani Afrika zinazohusika na uchumi wa baharini chini ya kauli mbiu "Afrika Tunayoitaka."
Akizungimza wakati wa kufungwa kwa kongamano hilo, mwakilishi wa Kenya katika jumuiya ya IGAD dkt Fatma Adan ametoa wito kwa serikali za bara Afrika kuwekeza zaidi katika utumizi wa raslimali za baharini badala ya kutegemea raslimali za nchi kavu pekee.
Aidha amepongeza hatua zilizopigwa kieneo katika kuhakikisha kunakuwa na mabalozi wa uchumi wa baharini.
Kwa upande wake, katibu katika idara ya Uvuvi na uchumi wa baharini Rodrick Kundu ametaja kuwa juhudi za kupiga hatua katika ukuzaji wa uchumi wa baharini zinapaswa kuanzia katika ngazi ya jamii.
Kundu ametolea mfano mradi unaondelezwa na jamii huko Kwale wa uvunaji wa hewa kaa, akisema serikali inalenga kuendeleza mradi sawa na huo katika maeneo mengine ya Pwani.


 

More Stories