Mahakama ya Juu imetupilia mbali uwezekano wa kuwa na vituo zaidi vya kupigia kura kuchunguzwa.

Wakili Otieno Ogolla alikuwa amemwandikia msajili wa mahakama akiomba kuchunguzwa kwa fomu 32A kutoka vituo 229 huku Njoki Mboshe akiomba kuchunguzwa kwa vituo 238.

Lakini akisoma uamuzi wa jopo la majaji ya saba, Jaji Isaac Lenaola amesema wana saa 48 pekee za kuchunguza vituo 15 vya kupigia kura ambavyo mahakama iliagiza hapo awali.

Katika agizo hilo, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ilipaswa kutoa nakala zilizoidhinishwa za fomu maalum kwa vituo 15 vya kupigia kura.


 

More Stories

Buriani jenerali Francis Ogolla

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo