Inspekta Jenerali wa Polisi Japhet Koome amepuuza barua ya muungano wa Azimio la Umoja kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu.

Siku ya Jumamosi, Azimio la Umoja liliiandikia ICC, ikiomba mahakama imchunguze IG Koome kwa uhalifu dhidi ya haki za binadamu.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari Jumapili, asubuhi, Koome amesema hatishwi na barua hiyo. Anaongeza kuwa kuondolewa kwake hakutazuia kazi ya polisi kuendelea.

Hata hivyo, Koome amewaonya wanasiasa dhidi ya kuwachochea wafuasi wao na uharibifu wa mali.

Kupitia kwa wakili wake Paul Mwangi, Raila aliorodhesha wanahabari wanane na waandamanaji tisa aliosema waliuawa na polisi wakati wa maandamano hayo.

Orodha hiyo pia ilijumuisha Wakenya wengine 20 ambao walijeruhiwa wakati wa maandamano ya Jumatatu na Alhamisi.