Kamati ya bunge la kitaifa ya utawala na usalama imeahidi kushughulikia maombi ya jamii ya wapemba uko Kwale ya kutaka kupewa uraia wa taifa hili.

Kaunti ya Kwale kuna jumla ya wapemba 3730 huku wakiwa zaidi ya 7000 pwani.

Wakiongozwa na Oku Kaunya mbunge wa Teso North kamati hiyo inatarajiwa kuwasilisha ripoti kamili bungeni ambapo baadae mapendekezo yatawasilsilishwa kwa rais Uhuru Rais ili kufanya maamuzi.

Kabinga Wachira ambae ni mbunge wa Mwea ameelza kuwa iliwalazimu kuzuru eneo la Kichakamkwaju uko Shimoni eneo bunge la Lungalunga kutathmini ombi la jamii ya wapemba kupewa uraia.

Ujio wa kamati hio kunajiri baada ya jamii hiyo kuwasilisha mswaada bungeni wa kuomba uraia.

Kulingana na Robert Waweru kutoka shirika la kitaifa la kutetea haki za binadamu ameeleza matumaini ya jamii hiyo kupata uraia.
Shaame Hamisi Makame ni mwenyekiti wa jamii hiyo anatarajia kuwa ujio wa kamati hiyo kutaleta mwelekeo ili jamii hiyo kutambulika rasmi nchini.

Jamii hiyo imekiri kupitia changamoto nyingi.