Wizara ya afya kaunti ya Kwale imeanzisha mpango wa kuwadunga chanjo wasichana wenye umri wa kati ya miaka 10 hadi 14 ili kuwakinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya uzazi.

Afisa wa afya umma katika hospitali ya Msambweni Fatma Bakari amesema kuwa mpango huo ulikuwa umesitishwa kwa muda kutokana na janga la corona.

Akizungumza katika eneo la Ukunda, Bakari amesema kwamba chanjo hiyo inawalenga wasichana wa shule walio katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa huo.

Wakati huo huo afisa huyo amedokeza kwamba chanjo hiyo inalenga kuwakinga wasichana dhidi ya virusi vya HPV vinavyosababisha saratani ya uzazi.

Kulingana na Bakari wasichana wanaoshiriki ngono wako katika hatari ya kuambukizwa virusi hivyo.