Tume ya kuajiri walimu nchini TSC imesema itaanzisha usajili wa walimu wote kwa mfumo wa kidijitali.

Mwenyekiti wa kitaifa wa tume hiyo Jamleck Muturi amesema usajili huo utarahisisha kuhifadhi taarifa muhimu kuhusu walimu kote nchini kwa ajili ya kumbukumbu za mbeleni.

Amesema kuwa hivi karibuni walimu kote nchini watalazimika kusajiliwa upya kwa mfumo wa kidijitali wa Biometric.

Amesema kuwa mfumo huo utasaidia kutatua baadhi ya changamoto wanazopitia walimu kama vile kupata baadhi ya huduma muhimu za dharura popote waliko badala ya kulazimika kusafiri hadi kwenye ofisi kuu za tume hiyo.

Vilevile amesema tume hiyo inaendelea kushughulika kuhakikisha kuwa walimu wanapostaafu wanapata malipo yao kwa wakati ufaao kinyume na ilivyo kwa sasa ambapo malipo hayo huchukua muda mrefu.

Wakati uo huo, amewataka walimu kukumbatia mabadiliko mbalimbali yanayotekelezwa na tume hiyo ili kufanikisha utendakazi wao.


 

More Stories

Buriani jenerali Francis Ogolla

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo