Kuna haja ya kuboreshwa kwa mazingira ya kikazi ya maafisa wa polisi kwa kupewa mafunzo zaidi na silaha za kisasa ili kupambana na wahalifu wa aina yoyote.

Mwanaharakati wa kijamii katika kaunti ya Lamu Yunus Is’haq amesema mara nyinyi polisi wanajipata katika mazingira magumu ya kikazi hasa wanapokabiliana na magaidi huku wakiwa hawana mahali pa kutoa lalama zao.

Amesema endapo maafisa wa polisi watakuwa na silaha madhubuti na ujuzi wa kisasa pamoja na kuongezwa mishahara na marupurupu ya watakuwa na motisha wa kazi hivyo basi kujitolea kikamilifu katika kutekeleza majukumu yao.

Aidha amesema ni jambo la kutamausha kwa taifa kupoteza maafisa wa polisi mikononi mwa wahalifu mara kwa mara akisema kuwa ni lazima serikali iboresha idara ya polisi.

Yunus ameyasema haya baada ya tukio la jana ambapo maafisa wanne wa GSU waliuwawa kwa kulipuliwa na washukiwa wa Al-Shabaab katika eneo la Milihoi kwenye barabara kuu ya Lamu-Garsen.

 


 

More Stories