Wasomi na viongozi wa dini ya kiisalmu kaunti ya Mombasa wameitaka serikali ya kaunti kutimiza matakwa ya wahudumu hao wa afya.

Wakiongozwa na Sheikh Abuu Hamza amesema wanaunga mkono hatua ya wahudumu hao kususia huduma zao na kwamba wana haki ya kugoma iwapo serikali ya kaunti imekataa kuwatimizia mahitaji yao.

Ameongeza kuwa serikali ya kaunti ya Mombasa inafaa kutekeleza matakwa ya wahudumu hao wa afya kama wanavyodai ikiwemo kulipwa kwa madeni ya mishahara yao, kupandishwa vyeo na kulipiwa bima ya afya ya NHIF.

Kiongozi huyo wa dini amesema iwapo serikali ya kaunti itadinda kutekeleza matakwa hayo, mwananchi wa kawaida anayetegemea huduma katika hospitali za umma atazidi kuumia.

Wakati uo huo, ameitaka serikali kuu kuingilia kati na kusuluhisha mgogoro unayoikumba sekta ya afya katika kaunti ya Mombasa.

 


 

More Stories

Buriani jenerali Francis Ogolla

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo