Wakazi katika eneo la Bamba kaunti ndogo ya Ganze wanaishi kwa hofu baada ya ndovu wengi kuonekana wakizurura katika maeneo mbalimbali. 

Wakazi hao wanasema vijiji ambavyo vimevamiwa zaidi ni vijiji vya Chira,Mnagoni Bandari na Mitsemerini. 

Daniel Kenga kiongozi wa maswala ya kimaendeleo katika eneo hilo amesema kwa sasa wananchi wanaogopa kurauka kufanya shughuli zao kwa kuogopa kuvamiwa. 

Mbunge wa Ganze Teddy Mwambire amesema amewasiliana na maafisa wa huduma kwa wanyama pori ambao tayari wameanza kuwafurusha ndovu hao hadi mbuga ya wanyama ya Tsavo Mashariki.

Mwandishi:Rose Tawa