Mgombea wa kiti cha wanawake kaunti ya Mombasa Zamzam Chimba Momhammed amemsuta vikali mgombea mwenza Amina Abdalla kwa madai kwamba amekuwa mstari wa mbele kuwasema vibaya wapinzani wake katika majukwaa ya kisiasa.

Trizer Odero na taarifa kamili

 

Kauli ya Zamzam inajiri baada ya Amina kumsuta mgombea wa ugavana kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir kufuatia hisia ya upendo aliyoitoa Nassir kwa wakaazi wa Mvita wakati wa hafla ya kutoa hundi ya basari kwa wanafunzi wa shule za upili katika ukumbi wa Lohana.

Kwenye hafla hio Nassir alionekana kububujikwa na machozi wakati akiwahutubia wakaazi wa eneo mbunge la Mvita.

Akizungumza na wakaazi eneo la Shanzu eneo bunge la Kisauni Zamzam amemtaka Amina ambaye anagombea kiti hicho kwa tiketi ya Jubilee kuepuka kuingilia viongozi wa vyama vyengine na badala yake aeneze sera zake.