Shirika la kutetea haki za binadamu la HAKI YETU chini ya vuguvugu la kitaifa la Angaza Movement limeitaka tume huru ya uchaguzi (IEBC) kwa kushirikiana na idara ya mahakama pamoja ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka ya Umma nchini kuwazuai wanasiasa wanaokabiliwa na tuhuma za ufisadi kuwania wadhfa wowote kwenye uchaguzi mkuu ujao.

 


Akizungumza na wanahabari katika kaunti hiyo Afisa wa maswala ya dharura katika shirika hilo Peter Kazungu amesema kuwa kuna viongozi wanaokabiliwa na kesi tofauti zikiwemo za mauaji na ufisadi ilhali wameruhusiwa kuweza kugombea viti mbalimbali vya kisiasa.


Kazungu ametaja hatua hiyo kwamba inchangia kwa kuchaguliwa viongozi wasiowajibika na kuzitaka idara husika kufutilia mbali vyeti vya wagombea kama hao hadi pale kesi dhidi yao zitakapoamuliwa.


Kauli ya Kazungu imetiliwa mkazo na mwanaharakati mwenza wa shirika hilo Julius Wanyama na kusema kuwa katu hawatakubali viongozi kama hao kuweza kuchaguliwa na wananchi.


Kwa upande wake Jamal Abdallah amekemea hali ya uchochezi ya kikabila ambayo imeanza kudhihirika katika maeneo tofauti hasa wakati huu wa kipindi cha uchaguzi.


Abdallah ameonya wanasiasa na mtu yeyote dhidi ya kujihusisha na chuki za kikabila na kwamba shirika hilo litawachukulia hatua za kisheria wachochezi wote.

Mwandishi: Ibrahim Juma Mudibo


 

More Stories

Buriani jenerali Francis Ogolla

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo