Sekta ya uchukuzi inazidi kupata pigo kutokana na kupanda kwa bei za mafuta nchini.

Kulingana na wadau katika sekta hiyo kupanda kwa bei ya mafuta mara kwa mara kumewaathiri sana kibiashara huku sheria ya uchukuzi ya kubeba asilimia 50 ya abiria ikizidi kuwaumiza.

Swaleh Athman mmoja mmoja wa wahudumu wa magari ya umma ameeleza kuwa mafuta yanapopanda wao wanalazimika kugharamika zaidi ilihali nauli bado inasalia ilivyo huku baadhi ya abiria wakitaka kupunguziwa nauli wanapoabiri magari.

Kwa upande wake Chaka Kombe dereva wa boda boda amedai kuwa kazi imekua ngumu sasa kutokana na gharama ya maisha akitaja ongezeko la bei ya mafuta kuathiri pakubwa mapato ya ya siku.
Haya yanajiri huku mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli nchini ikieleza ongezeko hilo la kila mwezi linatokana na kupanda kwa bei za kimataifa.

Sasa lita ya petroli inauzwa kwa shilingi 120 baada ya mafuta hayo kupanda kwa shilingi 7.63 zaidi, mafuta ya dizeli yakipanda kwa shilingi 5.75 huku ya taa yakipanda kwa shilingi 5.41.

Gharama ya petroli inayoingizwa kutoka nje iliongezeka kwa asilimia 14.97 katika mwezi uliopita wakati gharama za kuagiza dizeli na mafuta ya taa zikipanda kwa asilimia 12.29 na 13.26 mtawalia.

[Picha kwa hisani]