Wahudumu wa maboti ya abiria hasa yale ya mwendo kasi katika kaunti ya Lamu wanaitaka serikali kuwaruhusu kubeba idadi ya abira kama walivyokuwa wakibeba zamani kabla ya kuingia kwa janga la Corona nchini.


Wakiongozwa na Badi Nassir wahudumu hao wamesema hatua hiyo imeathiri spakubwa mapato yao hasa wakati huu ambapo bei ya mafuta ya petrol iko juu hivyo basi wakiitaka serikali kuwaruhusu kubeba abiria tisa kama zamani ili waweze kumudumu gharama za mafuta sambamba na kukidhi mahitaji yao.
Awali maboti hayo yalikuwa yakibeba abiria tisa kinyume na sasa ambapo yanabeba abiria sita pekee kwa kuzingatia kanuni za afya kuhusu kuzuia maambukizi ya Corona.
Aidha wamesema kuwa kiwango cha abiria pia kimepungua kutokana na kudorora kwa sekta ya utalii jambo ambalo wamesema limezidisha hali ya maisha kuwa ngumu na bado majukumu yanawakabili hasa wakati huu ambapo shule zimefunguliwa.