Washikadau katika sekta ya bahari, biashara na usafiri wamekutana kutafuta mikakati ya kufanya kanda ya Afrika Mashariki kuwa kivutio na yenye ushindani wakati ulimwengu unakabiliana na athari za ulimwengu za janga la Covid-19.

Wakizungumza wakati wa mkutano na viongozi wa ubaharia ulioandaliwa na halmashauri ya bandari nchini KPA kwa kushirikiana na baraza la kibiashara Kanda ya Afrika Mashariki, (EABC), wahusika wa sekta hiyo wametaka hatua za haraka za kuboresha biashara.

Kaimu mkurugenzi wa bandari balozi John Mwangemi amesema janga la Covid-19 limevuruga ugavi na kushusha uchumi wakati wazalishaji walipofunga biashara zao kutokana na vikwazo vilivyowekwa na serikali kudhibiti kuenea kwa virusi vya maradhi hayo.

Amesema kama bandari nyengine nyingi, bandari ya Mombasa imerekodi kupungua kwa idadi ya mizigo mwaka wa 2020 ambapo imeshindwa kusajili mizigo kupita tani milioni 34.12 ikilinganishwa na mwaka 2019.

Vilevile idadi ya makasha imepungua kwa asilimia 4 mwaka 2020 ikilinganishwa na mwaka 2019.

Akizungumza kwenye kikao hicho mwenyekiti wa baraza la kibiashara Kanda ya Afrika Mashariki, (EABC), Nick Nesbitt amesema janga la Covid-19 limechangia kwa kiasi kikubwa kiwango cha chini cha biashara na uwekezaji wa ndani ya jamii ya Afrika Mashariki.

Nesbitt amehimiza serikali za Afrika Mashariki kushirikiana na kuzitumia raslimali zao tajiri za baharini na nchi kavu kwa kuziboresha kabla ya kuzisafirisha katika mataifa ya nje kama chanzo cha ukuaji, ujumuishaji wa biashara na ustawi.


 

More Stories

Buriani jenerali Francis Ogolla

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo