Hatimaye muungano wa mabaharia nchini SUK waandaa uchaguzi wake

Hatimae Muungano wa mabaharia nchini SUK umeandaa uchaguzi wake rasmi katika ukumbi wa Licodep eneo bunge la Likoni kama ilivyoratibiwa baada ya uamuzi wa mahakama ya leba.Katika uchaguzi huo,...

Serikali ya kitaifa na kaunti zatakiwa kushirikiana kuwawezesha wavuvi kwa vifaa vya kisasa

Ipo haja ya serikali ya kitaifa na zile za kaunti kushirikiana kuhakikisha inawekeza zaidi kwa kuwawezesha wavuvi kupata vifaa kuvua katika bahari kuu.Gavana wa Lamu Issa Timamy ambaye pia ni...

Takriban wanafunzi 50 kutoka shule mbili za upili gatuzi dogo la Likoni wamenufaika na mradi wa kujifunza Kiingereza pamoja na ujuzi wa kimaisha.

Mradi huo wa Access unaofadhiliwa na Ubalozi wa Marekani humu nchini kwa sasa utawafaidi wanafunzi hao wa shule za upili za Mrima na ile ya Shika Adabu ukilenga kuwajenga wanafunzi hao kujiamini na kujieleza haswa kwa lugha ya Kiingereza pamoja na mafunzo ya kidijitali.

Kulingana na mkurugenzi mkuu wa shirika la Samba Sports Youth Agenda linalotekeleza mradi huo Mohammed Ali Mwachausa,wanafunzi kwa kipindi cha miaka miwili watawezeshwa kunoa lugha ya Kiingereza ili kuboresha hali yao ya kimasomo ikizingatiwa kuwa asilimia kubwa ya masomo yanatahiniwa kiingereza.

Kwa upande mwalimu wa Kiingereza wa shule ya upili ya Mrima Nancy Wambura anayesimamia mradi huo katika shule hiyo, ameeleza matumaini yake kwa mradi huo akisema utaboresha uwezo wa wanafunzi sio tu kimasomo bali vile vile kujenga ushujaa wa kujieleza mbele za watu pamoja na jinsi ya kuamiliana na wengine katika jamii.

Shaukan Ali, mwanafunzi wa kidato cha kwanza ambaye ni mmoja wa wale waliofaulu kujiunga na mradi huo anaeleza kuwa moja wapo ya matarajio yake ni kujenga uwezo wake wa kujieleza mbele za watu kwa kiingereza pamoja na kuwa mkakamavu.

Wiki hii wanafunzi hao wanasafiri hadi jijini Nairobi ambapo watafanya ziara katika sehemu mbali mbali ikiwemo bunge na kisha baadae kukutana na balozi wa Uingereza humu nchini.

Katika awamu ya kwanza ya mradi huo, shule za upili za Kombani na Ng’ombeni zilinufaika.

Mwandishi: Ali Mwalimu


RadioRahma ads