Tume ya IEBC imesema kuwa imeidhinisha wawaniaji 4 pekee kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao.

4 hao ni naibu rais William Ruto wa chama cha UDA, kiongozi wa ODM Raila Odinga, profesa George Wajackoya wa Roots Party na David Mwaure wa chama cha Agano

Kupitia mwenye kiti wake Wafula Chebukati, tume hio imesema kuwa wale walio na malalamishi wana nafasi ya kufika katika kamati ya kutatua mizozo ya tume hio.

Hata hivyo tume hio imebatilisha kuidhinishwa kwa Walter Mong’are wa Umoja Summit Party ikitaja tashwishi kuhusu shahada yake.