Mgombea kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir ametoa wito kwa mgombea wa urais wa muungano wa Azimio la umoja One kenya Raila Odinga na mgombea mweza wake Martha Karua kutoa fursa ya manfesto yao walioizindua hapo jana kuweza kusambazwa mashinani kupitia shirika la maendeleo ya wanawake.

Akitoa wito huo katika hafla ya kusherehekea miaka 70 ya tangu kuzinduliwa kwa shirika la maendeleo ya wanawake nchini,katika ukumbi wa chuo cha mafunzo ya kiserikali cha Kenya School Of Government hapa Mombasa Nassir amesema kuwa manfesto hayo yameangazia pakubwa masuala ya wanawake akieleza haja ya kusambwazwa mashinani wanawake wapate kufaidi.

Kulinga naye serikali ya Odinga na Karua imeweza kuweka njia mwafaka ya wale wanawake wajane na wasichana ambao waliacha shule kwa sababu ya mimba za mapema kuhakikisha kuwa wanapata elimu kwa manufaa yao ya siku za usoni.

Kwenye suala la miradi Nassir ameiomba serikali ya Odinga na Karua kuweka mikakati mwafaka ili kuona kuwa wanaweka miradi ya ujenzi wa mitambo ya kutengeneza Sodo ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa vifaa hivyo kwa wasichana hususan wanafunzi kike walioko katika shule mbalimbali nchini.

Hafla hiyo aidha imehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo mgombea mweza wa kiti cha urais chini ya muungano wa Azimio la umoja Martha Karua,gavana kaunti ya Kitui Charity Ngilu,mgombea wa ugavana kaunti ya Kilifi Gideon Mung'aro,mbunge wa Taveta Naomi Shaban,msemaji wa serikali Kanze Dena miongoni mwa viongozi wengine pamoja na wanawake kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa pwani.

 

 


 

More Stories

Vita dhidi ya mihadarati vyapamba moto Pwani

Fuo za bahari sasa ni marufuku

Ufunguzi wa shule waahirishwa kwa muda usiojulikana

Buriani jenerali Francis Ogolla