Mgombea wa ugavana kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir ametajwa kuwa na umaarufu Zaidi ukilinganisha na wagombea wengine wanaomezea kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa.

Hii ni kwa mjibu wa utafiti uliofanywa na shirika la utafiti la Infotrack nchini.

Kulingana na utafiti uliofanywa na shirika hilo walioufanya mnamo 27 Agosti mwaka huu kwa njia ya simu Nassir wa ODM ameibuka kidedea akiwa na asilimia 50

Shirika hilo lilifanya utafiti kwa kuwahoji wakaazi wa Mombasa kuwa ni nani watakaye mchagua kuwa gavana wao endapo uchaguzi utaandaliwa hii leo.


Aidha utafiti walioufanya Mwezi wa Julai mwaka huu ulionyesha kuwa Abdulswamad Shariff Nassir anaongoza akiwa na 50% akifuatwa na aliyekuwa mgombea wa kiti hicho Mike Mbuvi Sonko wa chama cha Wiper akiwa na asilimia 22,Hassan Omar Sarai wa chama cha UDA akiwa na asilimia 9 naye William Kingi wa chama cha PAA akiwa na asilimia 1.

Kadhalka katika utafiti uliofanywa na shiriki hilo mwezi huu wa August mwaka huu vile vile ulionyesha Abdulswamad Shariff Nassir wa chama cha ODM angali angali anaongoza kwa asilimia 50,Hassan Omar Sarai akiwa na asilimi 26,Omar Said Abdalla asilimia 1,Hezron Awiti Bollo akiwa na asilimia 0.5,William Kingi asilimia 0.2 naye Makazi Shafi akiwa na asilimia 0.1.

Na katika umaarufu wa vyama,shirika hilo lilibaini kwamba mnamo Julai mwaka huu chama cha ODM kiliongoza kwa umaarufu kikiwa na asilimia 51,UDA asilimia 20,WDM-K asilimia 2,chama cha JUBILEE kikiwa na asilimia 1 huku vyama vyengine vikiwa na asilimia 4.

Mnamo Agosti mwaka huu chama cha ODM kimeongoza tena kikiwa na asilimia 45 ya umaarufu,chama cha UDA kikiwa na asilimia 28 na vyama vyengie vikiwa na asilimia 1.

Haya yanajiri huku kaunti ya Mombasa ikiwa na jumla ya wapiga kura waliojisajili 641,913 huku eneo bunge la Changamwe likiwa na jumla ya wapiga kura 93,561, Jomvu 75,085,Kisauni 135,276,Nyali 124,253,Mvita 118,974,Likoni 94,764.


 

More Stories

Miraa na Mgoka kupigwa marufuku Mombasa

Wanafunzi kurudi shuleni juma lijalo

Vita dhidi ya mihadarati vyapamba moto Pwani