Huku zikiwa zimepita siku chache tu baada ya kuapishwa kwa gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir na naibu wake Francis Foleni Thoya sasa serikali ya kaunti Mombasa imeanza mikakati ya kuondoa kero la Mirundiko ya Taka.

Kwenye kikao afisini mwake na washikadau kutoka kwa baadhi ya kampuni za kibinafsi hapa mji Mombasa gavana wa pili wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir ametoa uhakikisho kwamba kero ya mirundiko ya taka mjini Mombasa sasa inaenda kuzikwa kwenye kaburi la sahau.

Kampuni hizo ambazo ziko chini ya chama Cha muungano wa ukusanyaji taka hapa Mombasa zilielezea ari ya kushirikiana na serikali ya kaunti ili kudumisha usafi wa mazingira.

Mbali na hayo Serikali ya kaunti Mombasa chini ya gavana Nassir inaendelea kupanga mikakati ya kuleta kampuni zenye kushughulikia ubadilishaji wa taka kuwa ni zenye kutumika Tena kwa manufaa ya wakaazi wa kaunti.

Njia hii ikitarajiwa kuleta ajira kwa wakaazi wa kaunti ya Mombasa.