Baadhi ya wabunge wa Azimio La Umoja One Kenya wanashinikiza kusitishwa kwa zoezi la kuratibu mipaka unaratibia kutekelezwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).

Wakiongozwa na Mbunge wa Ruaraka T.J Kajwang, wabunge hao ambao walikuwa wamefika makao makuu ya IEBC kupinga kusimamishwa kazi kwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji Ruth Kulundu, walisisitiza kuwa shirika la uchaguzi haliwezi kuendesha zoezi hilo ikizingatiwa sekretarieti yake inayumbayumba.

Viongozi hao walimkashifu Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa IEBC Marjan Hussein kwa kupuuza sheria katika utendakazi wa shirika hilo hali waliyosema imedunisha tume hiyo.

Wabunge wa muungano unaoongozwa na Raila Odinga walitishia kuchukua hatua kali dhidi ya Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati na Afisa Mkuu Mtendaji wa shirika hilo kwa kile walichokitaja kuwa na upendeleo.

IEBC ina jukumu la kuratibu mipaka ya maeneo bunge kwa kuongozwa na idadi ya watu na mambo mengine yaliyowekwa kisheria.

Kifungu cha 89 cha Katiba kinaitaka IEBC kukagua majina na mipaka ya maeneo ya maeneo bunge kwa vipindi visivyopungua miaka minane na isiyozidi miaka 12.


 

More Stories

Fuo za bahari sasa ni marufuku

Ufunguzi wa shule waahirishwa kwa muda usiojulikana

Buriani jenerali Francis Ogolla