Serikali ya kaunti ya Mombasa imeunda kitengo maalum cha kushugulikia masuala ya ukusanyaji ushuru.

Akizungumza na wanahabari afisini mwake gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir ameeleza kuwa kitengo hicho kitakacho shughulikia huduma za ukusanyaji wa ushuru katika kaunti kitasajiliwa kama shirika chini ya serikali ya kaunti Mombasa lengo na madhumuni likiwa ni kuendeleza huduma bora za ukusanyaji wa mapato ya kaunti.

Aidha afisa wa kaunti waliokuwa wakifanya shughuli ya ukusanyaji ushuru katika serikali ya kaunti iliopita wakipangiwa majukumu mengine.

Kulingana na Nassir amechukua hatua hiyo ili kupunguza lalama kutoka kwa wakaazi na wafanyibiashara katika maeneo mbalimbali ya kaunti ambao wamekuwa wakilalamikia kuhangaishwa na kusumbuliwa na maafisa hao.

Nassir amewataka wakaazi wa kaunti ya Mombasa kutarajia kuona huduma bora ya ukusanyaji wa ushuru pasipo na usumbufu.