Chama cha Madaktari Kenya (KMA) kimetoa ushauri kwa Wanawake wajawazito au au wanaonyonyesha wapate chanjo za COVID-19 ili kujilinga na ugonjwa huo.

KMA inasema kwamba data inaonyesha kuwa wanawake wajawazito wana uwezekano mkubwa wa kuambukizwa Covid-19 na wako katika hatari kubwa ya kufariki au kulazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Taarifa ya KMA inataja kuwa Wanawake wajawazito walio na shida zingine za kiafya wapo katika hatari kubwa ya ugonjwa mbaya.

Kuhusu mikusanyiko ya umma, KMA inapendekeza kwamba mikutano yote ya hadhara iahirishwe hadi Kenya ifikie kiwango cha chanjo cha 60% ya watu waliochanjwa.