Vifo vya watu wanaokufa kutona na corona nchini vimeongezeka hadi 4,497. Hii ni baada ya wagonjwa wengine 30 kufariki.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema kuwa kuna wagonjwa 2,063 kwa sasa wamelazwa katika vituo vya afya nchini , wakati 9,024 wako chini ya mpango wa Kutengwa na Huduma ya nyumbani.

Wagonjwa 149 wako katika Kitengo cha wagonjwa Mahututi (ICU), 77 kati yao wako kwenye msaada wa upumuaji na 72 kwenye oksijeni ya ziada.

Wagonjwa wengine 819 wako kando na oksijeni na 756 kati yao katika wadi za jumla na 63 katika Vitengo vya Utegemezi wa Juu (HDU).

Visa vipya 646 vya corona vimeripotiwa nchini ndani ya saa 24 zilizopita.

Wakati huo huo, wagonjwa 255 wamepona ugonjwa huo na 200 kutoka mpango wa Kutengwa na Huduma ya Kutumia Nyumbani wakati 55 kutoka vituo anuwai vya afya nchini kote.


 

More Stories

Fuo za bahari sasa ni marufuku

Ufunguzi wa shule waahirishwa kwa muda usiojulikana

Buriani jenerali Francis Ogolla