Chama cha kisiasa cha Umoja Summit hapa nchini kimesema kuwa kinaendeleza mikakati ya kusimamisha wagombea wa nyadhifa mbalimbali za kisiasa kote nchini.

Kiongozi wa chama hicho Naomi Cidi amebaini kuwa chama hicho kiko na wanachama wengi na akawataka wanasiasa wote kujiunga na chama hicho katika safari yao ya kutafuta uongozi.

Kulingana na Cidi,chama hicho kitaendeleza chaguzi za mchujo zenye uwazi na haki.

Wakati huohuo amewataka wapwani kuja pamoja na kuhakikisha kuwa wameunga mkono vyama vya kisiasa ambavyo vinamizizi kutoka eneo hili.

Hatua hiyo inajiri huku joto la kisiasa nchini likiendelea kupanda kila kukicha.