Mgombea wa  cha Urais nchini kupitia chama cha DP yaani democratic Party spika Justine Muturi amesema kuwa ataimarisha uchumi wa eneo la pwani iwapo wakenya watamchagua kuwa rais.

Akizungumza mjini Kilifi wakati alipokutana na jamii ya GEMA,Muturi amesema kuwa eneo la Pwani liko na raslimali nyingi ambazo zikiendelezwa vyema zitaimarisha uchumi.

Mgombea huyo wa urais amebaini kuwa atafufua viwanda ambavyo vilisambaratika miaka mingi iliyopita ili kubuni nafasi zaidi za ajira kwa vijana.

Wakati huohuo ametaja zao la mnazi kuwa moja wapo ya raslimali ya eneo la pwani ambayo inaweza kukabiliana na umaskini.

Ameongeza kuwa kuna haja ya kufunguliwa kwa viwanda vya kusafisha zao la mnazi ili kutengeneza bidhaa mbalimbali na kuziuza hapa nchini na hata mataifa ya nje.

 


 

More Stories

Fuo za bahari sasa ni marufuku

Ufunguzi wa shule waahirishwa kwa muda usiojulikana

Buriani jenerali Francis Ogolla