Chama cha United Democratic Movement (UDM) kinachounga mkono muungano wa Azimio-One Kenya Alliance kimesema kuwa kiko tayari kupambana na chama cha UDA katika kaunti ya Kwale.

Mgombea wa kiti cha wadi ya Bongwe/Gombato kupitia chama hicho Matano Rama amepuzilia mbali umaarufu wa chama cha UDA katika kaunti hiyo.

Rama amesema kuwa amejiandaa vilivyo kukabiliana na mpinzake wake wa chama cha UDA Tumaini Mwachaunga katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Kwa upande wake wafuasi wa mgombea huyo wameelezea matumaini ya kushinda kwenye uchaguzi huo baada ya chama cha UDM kumpatia tiketi ya moja kwa moja.

Wakiongozwa na Athumani Ali, wafuasi hao wamewataka wapinzani wao wa chama cha UDA kudumisha amani wakati wanapojitayarisha kwa uchaguzi ujao.