Huenda swala la kuzagaa kwa chupa za plastiki jijini Mombasa likazikwa katika kaburi la sahau baada ya makundi matatu ya kijamii kunufaika na vifaa vya kuchakatua chupa za plastiki.

Mashine hizo za kuchakatua taka za plastiki zimefadhiliwa na shirika la WWF Kenya kwa ushirikiano na wakfu wa CocaCola.

Kulinga na afisa mkuu wa utunzaji mazingira wa WWF Kenya Jackson Kiplagat chupa nyingi za plastiki zimezagaa kaunti ya Mombasa na pia katika fuo za baharini hali aliyoitaja kuchafua mazingira na kuhatarisha viumbe wa baharini.

Kwa upande wake waziri wa Mazingira kaunti ya Mombasa Godfrey Nato vifaa hivyo vitasaidia katika kulinda mazingira na pia kuongeza ajira miongoni mwa vijana wa Mombasa.

Wakati huo huo Juma Nondo Kusissa kutoka shirika la kijamii la Likoni Community For Development,ambaye ni mmoja wa wanajamii walionufaika na mashine hizo,amepongeza hatua hio na kusisitiza kuwa itasaidia juhudi zao za kulinda mazingira.


 

More Stories

Vita dhidi ya mihadarati vyapamba moto Pwani

Fuo za bahari sasa ni marufuku

Ufunguzi wa shule waahirishwa kwa muda usiojulikana

Buriani jenerali Francis Ogolla