Uingereza, viongozi wa dunia na wafalme kote ulimwenguni wanatarajiwa leo kuuaga na kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Malkia Elizabeth wa pili.

Saa kumi na mbili na nusu asubuhi ya leo muda rasmi wa kuutazama mwili huo unafika kikomo baada ya siku nne zilizoshuhudia maelfu ya watu wakisimama kwenye foleni ndefu kuuona mwili wa malkia huyo katika ukumbi wa kihistoria wa Westminster jijini London.

Mwendo wa saa tano jeneza lenye mwili wa Malkia Elizabeth litapelekwa hadi Westminster Abbey kwa ajili ya mazishi.

Miongoni mwa watu 2,000 watakaohudhuria mazishi hayo watakuwemo viongozi 500 wa dunia akiwemo rais wa Marekani Joe Biden, Mfalme Naruhito wa Japan, makamu wa rais wa China, Wang Qishan na rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa.

Vitukuu wa malkia, mwanamfalme George na binti mfalme Charlotte, watoto wawili wakubwa wa mrithi wa sasa wa kiti cha ufalme mwanamfalme William, pia watahudhuria.

Kwa hisani ya Dw swahili.


 

More Stories

Miraa na Mgoka kupigwa marufuku Mombasa

Wanafunzi kurudi shuleni juma lijalo

Vita dhidi ya mihadarati vyapamba moto Pwani