Wenye mahoteli sasa wanakila sababu ya kutabasamu baada ya watalii kuanza kumiminika katika hoteli zao baada ya kuondolewa kwa curfew.

Kulingana na meneja wa mikakati wa Masaai Beach Hoteli Josphat Iha tangu serikali iondoe “lockdown”watalii wa nje na wa humu nchini wameanza kuja kwa wingi, hivyo sekta ya utalii imeanza kunawiri kwa mpigo.

Ameongeza kuwa wanamatumaini kuwa sekta hio ya utalii itazidi kuimarika msimu huu wa sherehe za kufunga mwaka.

Kuhusu swala la kufuata kanuni za corona, Iha ametaja kuwa wanafuata kanuni zote za kujikinga na maambukizi ya corona kama ilivyoagiza wizara ya afya.