Wataalam wa mifugo kaunti ya Kwale wanahimiza wakulima wafugaji kukumbatia ufugaji wa mbuzi walioboreshwa aina ya Gala ili kujipatia faida kwa muda mfupi.

Samson Njenga mtaalam wa mifugo Kwale anasema kwamba aina hio ya mbuzi inastahimili ukame na magonjwa ikilinganishwa na mifugo wengine.

Njenga akipigia mfano wa zaidi ya ng"ombe na kondoo elfu 3 walioangamizwa na makali ya kiangazi miezi miwili iliyopita kaunti ya kwale huku mbuzi wakistahimili makali hayo.

Kwa upande wake Zachariah Mwasaru amewashauri wafugaji kutumia msimu huu wa mvua za vuli kuhifadhi chakula cha mifugo ili kuona kwamba hawaathiriki wakati wa kiangazi.

Aidha amewataka wafugaji kuhakikisha mifugo wao wanapata chanjo dhidi ya maradhi msimu huu ambapo mvua za vuli zinaendelea kushuhudiwa.

 

 


 

More Stories

Fuo za bahari sasa ni marufuku

Ufunguzi wa shule waahirishwa kwa muda usiojulikana

Buriani jenerali Francis Ogolla