Kongamano la kujadili uchumi wa baharini lakamilika huku hamasisho zaidi zikitolewa kupiga jeki juhudi hizo

Kongamano la kujadili mbinu za kuboresha uchumi wa baharini baina ya mataifa wanachama wa IGAD limekamilika rasmi hapa jijini Mombasa.Kongamano hilo la siku nne liliwaleta pamoja wawakilishi kutoka...

Serikali ya kitaifa na kaunti zatakiwa kushirikiana kuwawezesha wavuvi kwa vifaa vya kisasa

Ipo haja ya serikali ya kitaifa na zile za kaunti kushirikiana kuhakikisha inawekeza zaidi kwa kuwawezesha wavuvi kupata vifaa kuvua katika bahari kuu.Gavana wa Lamu Issa Timamy ambaye pia ni...

Aliyekuwa mgombea mwenza wa mfanyibiashara Suleiman Shahbal, Selina Maitha katika kinyang’anyiro cha kiti cha ugavana amezungumza kwa mara ya kwanza hadharani kuhusu sababu zake za kujiunga na chama cha UDA tangu Shahbala kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho na kumuunga mkono Abdulswammad Shariff Nassir.

Selina, akizungumza kwa mara ya kwanza katika mkutano na wafuasi wa chama hicho, amesema hajutii uamuzi wake uliosababishwa na msukumo wa kutaka mageuzi katika kaunti ya Mombasa.

Ameeleza kuwa haikuwa uamuzi rahisi kuamua mrengo atakaojiunga nao, akiahidi kuwa katika baadhi ya mirengo alikaribishwa kwa masharti ya kuhakikisha analeta kura.

Selina amesisitiza kuwa ari yake ya kutaka mageuzi itaendelea katika chama hicho cha UDA na wala hatojiingiza katika siasa za matusi.

Katika mkutano huo ulioandaliwa kwenye makao makuu ya Hustler Centre hapa Mombasa eneo la Nyali, wafuasi wa chama hicho wamempendekeza Selina kuwa mgombea mwenza wa mwaniaji kiti cha ugavana kupitia UDA Hassan Sarai.

Viongozi wa chama hicho wameahidi kuanza rasmi kampeni zao za kutafuta kura tunapoelekea katika uchaguzi mkuu mwezi Agosti.


RadioRahma ads