Mwendazake aliyekuwa raisi wa tatu wa taifa la Kenya Mwai Kibaki ametajwa kuwa raisi aliyejali pakubwa maslahi na haki za watu wanaoishi na ulemavu.

Kibaki amesifiwa kwa kutia saini kuwa sheria miswaada ya kutetea haki za watu wenye ulemavu pamoja na kuanzisha mfumo wa kuwapa watu wenye ulemavu fedha za kila mwezi.

Kulingana na wasimamizi wa shirika la wanawake jijini Mombasa la Tunaweza Women With Disability,wakiongozwa Charity Chahasi wametaja kuwa taifa limepoteza shujaa aliyejali haki za walemavu.

Wakati huo huo Chahasi ametaja kuwa Kibaki aliweza kukuza uchumi wa taifa hili,kinyume na maraisi waliomtangulia.

Kwa upande wake afisa katika shirika hilo,Lucy Chesi amemtaja Kibaki kuwa aliyekuwa mcheshi na mpenda kufanya utani alipokuwa jukwaani.

 


 

More Stories

Fuo za bahari sasa ni marufuku

Ufunguzi wa shule waahirishwa kwa muda usiojulikana

Buriani jenerali Francis Ogolla