Rais Uhuru Kenyatta ametangaza nyongeza ya kima cha chini cha mshahara kwa wafanyikazi wa Kenya.

Akizungumza wakati wa sherehe za Siku ya Wafanyakazi katika uwanja wa Nyayo, rais ametangaza kuwa kima cha chini cha mshahara kimeongezwa kwa asilimia 12.

Agizo hili litaanza kutekelezwa leo, Jumapili, Mei 1, 2022.

Kwengineko Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga wamewaenzi wafanyikazi wa Kenya wakiadhimisha sherehe za siku ya Wafanyakazi kote nchini.

Katika ujumbe wake, Ruto amekiri jukumu muhimu ambalo wafanyikazi wa Kenya wameathiri uchumi akisema wameifanya nchi kuwa kama ilivyo.

Kupitia kwenye ukurasa rasmi wa twitter kinara wa ODM amewaahidi wafanyikazi malipo sawa katika utawala wake endapo atachaguliwa kuwa Rais katika uchaguzi wa Agosti 9.

Huku hayo yakijiri Katibu Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi Francis Atwoli bado amefutilia mbali kustaafu kwa Rais Uhuru Kenyatta kutoka kwa siasa.

Akiongea Jumamosi kabla ya sherehe za siku ya wafanyikazi katika zifuatazo, Atwoli amefutilia mbali uwezekano wa sherehe hizo kuwa za mwisho za Uhuru.

Amesema Uhuru hatakuwa rais wa kwanza duniani kuacha siasa kwa muda na kurejea tena baada ya muongo mmoja.