Maelfu ya watoto wameachwa bila ya makazi huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, eneo ambalo jeshi la taifa linakabiliana na waasi wa M23.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF limesema zaidi ya watu 190,000 nusu yao ikiwa ni watoto, wamelazimishwa kuvikimbia vijiji vyao katika maeneo ya Rutshuru na Nyiragongo.

Akizungumza baada ya ziara yake katika wilaya ya Rutshuru ya jimbo la Kivu ya Kaskazini, mwakilishi mkazi wa UNICEF kwa DRC, Grant Leaity amesema maelfu ya watoto wapo katika mazingira hatarishi na uhaba mkubwa wa mahitaji ya msingi ya kunusuru maisha yao.

Kundi la M23, lenye wanachama wengi wa jamii ya Watutsi ambalo lilisambaratishwa 2013, hivi sasa limerejea tena, likilishambulia jeshi la DRC na walinda amani wa Umoja wa Mataifa, na limefanikiwa kuyadhibiti maeneo kadhaa.


 

More Stories

Fuo za bahari sasa ni marufuku

Ufunguzi wa shule waahirishwa kwa muda usiojulikana

Buriani jenerali Francis Ogolla