Unyunyuziaji maji mashamba Kwale ndio suluhu la kukabili baa la njaa
Gavana wa Kwale Fatuma Achani amesema kuwa uzinduzi wa mradi wa kisima cha maji katika eneo la Melikubwa huko Macknon unalenga kukabiliana na baa la njaa katika eneo hilo ambalo hukumbwa na kiangazi kikali mara kwa mara.